Asilimia 99 ya tunachofundishwa shuleni kinatumika mtaani

“Tuna maadui watatu nchini mwetu, Umasikini, Magonjwa na Ujinga”Mwalimu Juilius Kambarage Nyerere

Katika pitapita za WhatsApp status za watu nilikutana na hiki kibonzo hapa chini. Nikacheka sana.

“Kila nikikumbuka kwamba na mimi niliwahi kuchanganua Sentensi kwa njia ya matawi nguvu zinaniishia” – @cheka_tu_ meme lord

Wakati nacheka nikakumbuka na mimi pia ni mhanga wa hii kitu. Nimesoma kuchambua matawi ila sasa mbona siitumii ?

Nikafuatilia mtandaoni nikajua kuwa elimu ya kuchanganua sentensi kwa matawi ni kitu ambacho dunia sasahivi inafanya na inatafta wataalamu wa kuchanganua kwa matawi kwa nguvu.

Mfano mmoja Apple inatumia kuchanganua matawi kuunda bidhaa yao inaitwa Siri , bidhaa inayo elewa ukizungumza kiingereza na inakujibu kama binadamu na inaingiza mabilioni ya pesa

Simu ya iPhone inavyotumia Kuchanganua sentensi kwenye bidhaa inayo iita Siri

Ukitaka Roboti lielewe Kiswahili, Lazima ulifundishe, Ukikata kulifundisha roboti Kiswahili Unalifundisha kwa kuchanganua sentensi kwa Matawi.

“Elimu sio njia ya kukwepa umasikini, Ni njia ya kupambana nayo”

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Tunachosahau ni kuwa sisi ni wachanga kwenye kila sekta.

Tunatoka shule na madini kichwani. Tunatafuta sehemu pa kutumia hayo madini, Hapo ndio kosa kubwa sana tunalofanya Kwanini?

Unafundishwa IT chuoni Alafu unaishi kwenye nchi ambayo asilimia 75 ya wananchi ni wakulima. UTAISHIA KULIMA MATIKITI TU Yani watu 8 kati ya 10 wanalima, Yani hata kama hutaki utalima tu .

Sasa ebu tujaribu ebu jiulize Wakoloni walivyokuja kwetu, walifanyaje?

Mwenzetu aliekuja TZ na ujuzi wa kuchambua pamba ziwe nguo akakuta watu wanavaa majani, Je alivofika alisema “Mbona nilichosoma haki tumiki huku?”

Je alieanzisha Benki ya kwanza Tanzania alisema “duuh mbona hii kitu haki apply BONGO watu wanatunza kwenye vibubu”?

HAPANA

Amazon, Ebay, Google na Yahoo zilianzishwa kipindi ambacho chini ya asilimia 1% tu ya wamerakani walikuwa na uwezo wa kupata Internet. Je walikaa kusema Google haifai kipindi hiki watu wenyewe hawana hata mtandao?

Mtu wa kwanza kutengeneza gari alisema “Ningekuwa naangalia mazingira yalionizunguka na kuuliza watu wanahitaji nini , nisingevumbua gari, ningetafuta farasi mwenye mwendokasi zaidi”

Hii akili inaitwa Ukorofi wa Kijasiriamali . Ni kitu sisi hatuna kabisa….

Wenzetu hawa hua wanasema “Dunia itafanya kwa njia nayotaka mimi na Sio kwa njia mlioizoea nyie”

Wenzetu wanafanya kitu kinaitwa Ku-uhisha mazingira. Kwa kiingereza ni “TRANSCENDED YOUR ENVIRONMENT

“Elimu inatakiwa iwafanye muwe wadadisi, na muwe na kiu ya kufahamu mambo…..Ninataka vijana wangu wawe sababu ya kumkosesha mkoloni usingizi.”

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Pata picha Elon Musk angefungua kampuni ya gari yanayotumia Mafuta. Je ni nani angeunda gari la kuchaji linalotembea lenyewe?

Kuna aliesoma Uhasibu na Shahada za kufa mtu ila akashindwa kumuelimisha mama yake atunze esabu za kuku wake kihasibu. Kila siku mama anaibiwa pesa na hawezi pata mkopo benki.

Yupo aliesomea Marketing na degree anayo ila hata kumuelekeza Baba yake atumie Facebook kutangaza biashara hawezi.

Mwingine amesoma Artificial Intelligence, Ila steshenari yake ya kuchapa barua. Anashindwa kutumia huo ujuzi kufundisha kompyuta ichape yenyewe.

Tuonaona shida sana kueneza elimu na kuitumia. Tunaishia kukubali hali iliyopo na tunatupa Cheti na tunnaenda kufanya wanachofanya watu tangu enzi na enzi kwa sababu ndio unakiona kinachofaa .

Mazingira yana nguvu sana, yani ni kweli huwezi ishi nchi ambayo 75% Ni wakulima alafu usilime. Wayahudi wengi wanafanya biashara ndio mana hata mtoto wa kiyahudi akizaliwa wanajua huyu lazima awe mfanya biashara (mfano Wanaomiliki Facebook). Myahudi asili yake sio kilimo.

Nachosema ni asili yetu ni kilimo ,hata ukiwa na cheo gani utashangaa unalima tu.

So ukipata ela kidogo utashangaa Moyo unakuvuta ukalime . Ukitaka kuwekeza huwazi teknolojia..unalima. Ukiwa na shida na ela huwazi ujasiriamali wengine zaidi ya kulima,ufugaji.. kwa kuwa ndio asili YAKO

Kulima sio vibaya , Ubaya ni unalima wewe alafu mwingine anakupangia bei. Na tukitaka kuondokana na haya lazima tuwe tunatumia tusomacho vyuoni.

Wanaopanga bei Wanataka kupunguza gharama ya chakula iwe yani chakula kisiwe na gharama yoyote. Wameweza kutengeneza kuku maabara. Sasahivi wana mboga majani yenye ladha ya nyama choma!!

Hatujifunzi wala kujitahidi ku-uhusha mazingira yetu, ndio maana hata kama tuna elimu, bado tunaishi kwa tamaduni zilizopo na tunafanya biashara za tamaduni zetu

Mzungu anaweza kuja leo nchini kwetu, Kitu kinaitwa “Uba” au “Uber” na aka tuaminisha tukitumie na tusipande taxi au bodaboda na tukakubali. Kwa sababu anajua ku-uhisha mazingira.

Jirani yako anachoma takataka kwa moto moshi mkali. Umesomea Mazingira ngazi ya Shahada ya Uzamilifu, na pia Sheria za Tanzania zinakulinda ila unashindwa kumkaripia kisa atakuloga au ni rafiki ya baba yako.

Wenzetu pia wana shida hii hii. Ila wanajua ku-uhisha mazingira

Mfano, Kuna kipindi watu hawakua wanapiga mswaki hadi wawe wanamatatizo ya meno. Ila Colgate ikaweza ku-uhisha mazingira hayo hadi watu wakawa wanatumia kila siku.

Nimegundua tunafeli kujifunza jinsi ya kuuhisha mazingira na kwahiyo tunafata tamaduni zetu kwenye pointi ambayo inatuumiza sisi wenyewe

Oy, mida mazee Acha Nikafatilie kama kuku wangu wame kula

โœŒ๐Ÿผ

Asante kwa kuipitia makala hii

Waweza kuni follow kupitia

Instagram : nickyrabit

Twitter : nngailo

Barua Pepe : nickyrabit@gmail.com

LinkedIn: Nicholaus Legnard

Related Posts

One thought on “Asilimia 99 ya tunachofundishwa shuleni kinatumika mtaani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *