Jenerali wa vita mkuu kuliko wote duniani

Hapo zamani za kale palikua na mfalme mmoja. Siku moja akaita watu wote kwenye falme yake akawaambia “Nileteeni mtu ambaye ni Jenerali wa vita bora kuliko wote hapa duniani”.

Kati ya hao wananchi waliomsikia, kuna mzee mmoja akamjibu mfalme “Mfalme wangu, Jenerali mkuu kuliko wote alisha fariki, akaenda mbinguni”

Mfalme akaona isiwe shida, akaenda mawinguni. Alivyofika akakutana na Petro amesimama mbele ya mlango wa mbinguni.

Mfalme akamwambia Petro, “Nimeelekezwa kuwa Jenerali mkubwa wa vita bora kuliko wote yupo huku na japo kuwa siwezi rudi nae duniani , ninaomba angalau kumuona”

Petro akamtizama kwa muda kisha akaaamua kumuonesha na kusema “yule pale”.

Mfalme akamuangalia akashangaa akasema “Huyu mbona namjua, huyu si alikua tu fundi wa viatu tu? Huyu sio Jenerali”

Petro akamjibu akasema “Ni kweli , ila huyu angekua ni Jenerali, ndio alikua Jenerali mkuu kuliko wote.”

Asante kwa kusoma 🙂

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *