Mambo 8 ya kufanya kabla hujalipia matangazo ya Youtube

“Youtube ni tovuti ya pili Tanzania nzima kwa kutizamwa”

Kama una channel yako Youtube au unataka kujitangaza kwa njia ya video, basi Youtube ni sehemu nzuri sana ya kutangaza.

Youtube ni website na app ya pili Tanzania nzima kwa kutizamwa. Hii ni ishara tosha kuwa uamuzi wako ni sahihi kabisa.

Sasa japo unashauku la kuanza kutangaza , Kuna mambo ya kuzingatia hapa kabla hujatangaza

Hakikisha video zako zina muonekano ubora wa hali ya juu

Kwa muuonekano, nina maanisha video yako haina chenga chenga, sauti imekaa vizuri imeandaliwa vema. Kuna viwango vya ubora wa video mfano HD, 4K Ila jitahidi video yako iwe ni HD au High Definition .

Simu nyingi sikuhizi zinaweza kutoa huu ubora kama hauna angalau Azima. Hawa Youtube wanataka kitu ambacho mteja wao akiingia atafurahia

Jaza taarifa zote ambazo Youtube wanataka ujaze

Kuna vitu vingi vya kujaza hua watu wanapuuzia mfano

sehemu imeandikwa “Description” yani sehemu ya kuweka maelezo ya video yako. Ni vema ukajaza kwa kirefu kuhusu video yako na pia ni vema Zaidi ukaelezea video yako kwa ufupi kabisa kwa kutenga kila wazo katika sentensi moja.

Jaza mawasiliano yako yote kuanzia namba za simu na njia zingine wanaweza kukupata.Na pia maelezo yako yawe na maneno ambayo yanaendana  na video yako ili mtu akitafuta neno, Youtube iwe inakusaidia kukutangaza na kukuweka uonekane

Jaza “tags” zote, na ziwe zinaendana na hiyo video yako

Kuna sehem uinaitwa tags ni kama hashtags za instagram (zile zenye #) ila huku unaweka neon au sentensi inayohusiana na video yako . mfano kama ni ujasiriamali….ukiweka tag kama “biashara”, “mikopo”, “vyuma vimekaza”…video itakua inahusiana vizuri na mtu unaemlenga

Ila Ukiwa umeandika “tag” mfano “Diamond Platnumz” wakati wewe ni biashara….japo diamond platnumz ni mtu anaeangaliwa Zaidi ya mara milioni moja kwa mwezi, video yako haitakuwa na muitikio mzuri kwa sababu watu wanaomtafuta Diamond wanataka burudani alafu wewe unawaletea mambo ya kubana pesa.

Hivyo Youtube ikijua tu hii video imewekwa sehemu siyo…inakushusha chini utakua huonekani kabisa

Usiweke wimbo au video clips zenye Hatimiliki bila ruhusa ya mhusika.

usieke nyimbo zenye hatimiliki kwa sababu watakufungia channel na kuchkua video zako pindi mtu mwenye hatimiliki yake akikutafuta

kuna nyimbo ambayo hazina hatimiliki uzi tafte uweke , mfano wa sehemu za kutafuta ni hapa https://www.bensound.com/

Hatimiliki ni kitu muhimu cha kuchunga. Kitaku gharimu ukipuuzia

Waweza kuongea na watu wengine ili uonekane kwenye Video zao

Muda mwingine sio lazima utumie pesa kulipa hawa Youtube kuna njia nyingine inaweza kugharimu pesa ndogo zaidi au hata bure.

Mfano, Unawatafuta watu wenye chaneli zinazoendana maudhui na wewe pia ambao mna idadi inayolingana ya Subscribers au fansi alafu mnakubaliana yeye akupe tangazo lake na wewe umpe lako mnabilishane mtangaziane kweye chaneli zenu. Au hata akikataa akitaka pesa nadhani pesa haitakuwa kubwa sana kulingana n Youtube

Hwa watu kwa kingereza inaitwa influencer marketing au affiliate…ni watu wenye ushawishi mkubwa. na sio lazima watu wakubwa sana yani, tafuta hata mtu mwenye video zake zenye views hata 100 zinakusaidia. 100 ni namba kubwa sana

Cha msingi tu utafute watu mnaoendana fansi au watizamaji au maudhui yanayoendana , mfano unaongea issue za ujasiriamali bas tafta channel za kuendana nahii kitu au ukitangaza kne channel za udaku na hiyi tangazo likae ivo ivo.

Wakumbushe watu wa subscribe (wajiunge)

Subscribe inatamkwa SABU-SKLAIBU. Maana yake ni wale watu waliojiunga kwenye chaneli yako. Siku ukiweka video yako mpya basi watataarifiwa kuwa umeweka kitu kipya hii inasaidia sana kuongeza fansi na idadi ya viewers au watizamaji.

Ukiwa na fansi wengi, waweza kuwa na watizamaji wengi kuliko hata baadhi ya redio na TV za kitanzania hapa

Panga video zako vizuri

Kuna kitu kinaitwa Playlist na ni njia ya kukusanya video zako kwenye makundi maalum ambayo unayapa jina moja.

Kitumie kupaga videos zako vizuri. Yani unaweza kukusanya video za Mapishi ya nyama ukakusanya zote ndani ya Playlist Moja

Uwe na muda maalum wa kuweka video zako hewani

Hii itakusaidia kuwapa fansi au watizamaji wako waje ku subsbribe kwa urahisi maana unawaambia “Subscribe ili uweze kupata mapishi mapya kila Ijumaa saa kumi jioni ili uwahi kununua viungo sokoni Jumamosi na kupikia wanao”

Hii inasaidia tu mtu anajua “leo saa mbilii jamaa anaachia kitu kipya ngoja nikamcheki”

Fungua akaunti za benki tofauti na ya mshahara , biashara au matumizi binafsi

Usifanye miamala ya kimtandao kwa kutumia kadi ya benki ya mshahara. iko siku utaja lia machozi. Tafuta akaunti ya tofauti kabisa..Au tumia hizi Masterpass kutoka huduma za mitandao ya simu. Mimi binafsi napendelea Equity bank kwa sababu ni fasta tu unajisajili

Natumaini umepata kitu kitakachoweza kukusaidia hapa .Asante sana kwa kusoma. Nitakuja tena kuelezea mbinu za kutengeneza matangazo ya Youtube ili yawe vizuri.

Karibu sana

Related Posts

2 thoughts on “Mambo 8 ya kufanya kabla hujalipia matangazo ya Youtube

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *